WANANCHI wa Mkoa wa Morogoro, wameondokana na mzigo wa gharama za kufuata vipimo vya CT-Scan mikoa ya jirani, baada ya Serikali kufikisha huduma hiyo katika hospitali ya mkoa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).
Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa mionzi mkoani humo, Emmanuel Mkumbo, akielezea maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya, tangu alipoingia madarakani Machi 2021.
Dk. Mkumbo amesema kabla ya mashine hiyo kufikishwa hospitalini hapo, kila mwaka wananchi kati ya 850 hadi 900 waliingia gharama za kuifuaga huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam au Hospitali ya Benjamin Mkapa.
“Mashine hii inatusaidia sana sababu tuna wastani wa wagonjwa 850 hadi 900 kwa mwaka wanaofanyiwa kipimo cha CT-Scan. Kabla ya kipimo hiki hakijaletwa tulikuwa tunapata shida kutambua magonjwa yanayotokana na mifupa na ajali mbalimbali,” amesema Dk. Emmanuel.