DOTTO BITEKO AITAKA TLS KUENDELEZA MSHIKAMANO NA KUISHAURI SERIKALI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania, Dotto Biteko, ametoa wito kwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuchagua viongozi watakaolinda mshikamano wa chama hicho.

Aliwasihi wanasheria hao kuchagua viongozi wenye kiu ya kuishauri na kuikosoa serikali, jambo ambalo TLS imekuwa ikilifanya.

“TLS mnalo jukumu kama chama kuchagua viongozi watakaoendeleza mshikamano wa chama chenu, watakaokuwa na kiu ya kuishauri na wakati mwingine kuikosoa serikali, jambo ambalo mmekuwa mkilifanya, naamini mtakuwa na viongozi ambao watakuwa na matamko ya kitaaluma.

Biteko alisisitiza umuhimu wa viongozi hao kutoa matamko ya kitaaluma na kuendelea kusisitiza umuhimu wa kuzingatia taaluma yao kama wanasheria, ambapo amenukuliwa akisema ” nitoe wito kwa chama kuendelea kuwa na msisitizo wa kukaa kwenye taaluma yenu kama wanasheria”

#KonceptTvUpdates

Related Posts