Washindi CRDB Marathon kuvuna mamilioni

WASHINDI wa Mbio za CRDB Bank Marathon 2024 zilizopangwa kufanyika Agosti 18 jijini Dar es Salaam, watazawadiwa jumla ya Sh 98.3 millioni.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CRDB, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa alisema wameamua kuweza zawadi nono kwa washindi kutokana na kutambua thamani ya washiriki na hadhi ya mashindano ambayo kwa sasa yamevuta mipaka ya nchi.

Alisema kuwa katika mbio hizo ambapo zitaongozwa na Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati, Doto Biteko, washindi wa kwanza kwa kilomita 42.2 watazawadiwa Sh10 milioni kila mmoja wakati washindi wa pili watazwadiwa sh5 milioni na washindi wa tatu watapata Sh2 milioni.

Pia kuakuwa na zawadi za washindi wanne hadi wa sita na kwamba endapo washindi watakuwa kutoka nchi za kigeni, benki yao itawazawdia Watanzania ambao wataoongoza katika orodha ya washindi ambao kila mmoja atazapata Sh2 milioni.

Alisema kwa upande wa nusu Marathon, washindi wa kwanza watazawadiwa Sh5 milioni, huku wa pili atapata Sh 2 milioni na watatu atazawadiwa Sh1 milioni katika mbio hizo ambapo Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL)ni mshirika.

Kwa upande wa mbio za kilomita 10, washindi wa kwanza watazawadiwa Sh2 milioni ambapo wa pili na wa tatu watazwadiwa Sh300,000 na Sh150,000. Pia kutakuwa na zawadi ya mshindi wanne mpaka wa sita.

Kwa upande wa mbio za baiskeli za kilomita 65, Mwambapa alisema kuwa watakuwa na zawazadi aina mbili ambazo ni za fedha taslimu na malazi katika hoteli ya nyota tano. Zawadi hizo oia zitakawahusu washindi wa mbio za kilomita 10.

Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli atazawadiwa Sh 3 milioni, mshindi wa pili Sh 1.5 milioni na wa tatu Sh1 milioni.

Kwa washindi wa mbio za kilomita tano, wa kwanza atapata vocha ya chakula cha mchana kwa watu wawili chenye thamani ya Sh250,000 pamoja na vocha ya Sh 500,000 itakayomruhusu kununua vifaa vya michezo katika duka la Shadaka Sports Wear.

Pia kutakuwa na zawadi  maalum kwa watoto watakaojishindia baiskeli na vifaa vya michezo ya watoto zenye thamani ya sh1, pamoja na  kufunguliwa akaunti za Junior Jumbo itakayowekwa Sh 500,000.

Mbali ya Tanzania, mbio hizo za msimu wa tano, zitafanyika kwa mara ya kwanza zitafanyika pia katika nchi ya DR Congo Jumapili na Burundi Agosti 11.

Alisema jumla ya washiriki 1,127 wa DR Congo wamekwishajiandikisha hadi sasa na kwa Burundi wamefikia  891 kwa mbio za Tanzania jumla ya washiriki 5,583 wamejisajili kati ya washiriki 8,000 wanaotarajiwa kushiriki mbio hizi na 823 ni raia wa kigeni.

Mwambapa alisema mwaka huu pia wameleta vifaa vya kisasa zaidi  na kuzifanya mbio hizo kuwa na utofauti kidogo.

Related Posts