Baiskeli kuliamsha Twenda Butiama | Mwanaspoti

MSIMU mpya wa kampeni ya Twende Butiama, umezinduliwa jijini Dar es Salaam huku, ikielezwa kwamba msafara wa baiskeli wenye lengo la kumuenzi na kuonyesha historia ya Baba wa Taifa, Mwl JK Nyerere utaamsha kampeni hizo za kila mwaka.

Kampeni hiyo inaendehswa na Kampuni ya Vodacom na msafara wa baiskeli utakuwa ni wa wiki mbili kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 13 mwaka  huu, ukianzia jijini Dar es Salaam hadi Butiama ikijumuisha wanaotoka nchi za Kenya, Rwanda, Burundi, Congo, Malawi na Zimbabwe.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkuu wa msafara, Gabriel Landa alisema kwa mwaka huu wanategemea kupata washiriki zaidi ya 200.

Landa alisema lengo la msafara huo ni kumuenzi baba wa taifa kwa vitendo huku ukipita sehemu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii kwenye upande wa elimu, afya na mazingira.

“Tunategemea kufika Butiama Novemba 13 ili tuweze kushiriki kumbukizi hiyo ambayo kilele chake ni Oktoba 14, tumelenga vitu vitatu elimu, mazingira na afya ambavyo Muasisi wa taifa alikuwa akivitilia mkazo,” anasema na kuongeza

Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, Zuweina  Farah amewaomba watu kujitokeza kwa wingi kuunga mkono uhamasishaji wa mazingira, afya na elimu.

“Kilichotushawishi kuingia kudhamini ni mambo matatu ya msingi yaliyopo kwenye kampeni yao, elimu, afya na kutokomeza umasikini, ukiachana na hilo washiriki watapata nafasi ya kuona uoto wa asili pia pesa watachangia ununuaji wa madawati kwa shule zenye uhitaji,” alisema Zuweina.

Related Posts