Stesheni za SGR zapewa majina ya marais, Dar yaitwa Magufuli

Dodoma. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa majina ya vituo vya stesheni za treni ya umeme (SGR) kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma.

Majina ya vituo hivyo ni ya marais wastaafu ambao, Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete, John Magufuli, Abeid Aman Karume na yeye mwenyewe (Samia).

Rais Samia akihitimisha hotuba yake ya uzinduzi leo Alhamisi, Agosti 1, 2024 amesema, stesheni ya Dar es Salaam: ‘Imepewa jina la Magufuli, stesheni ya Morogoro itaitwa Kikwete.”

Rais Samia ameridhia Stesheni Kuu ya Dodoma sasa itaitwa Stesheni ya Samia, Tabora itaitwa Stesheni ya Mwinyi, Stesheni ya Shinyanga itaitwa Karume, Stesheni ya Mwanza itapewa jina la Mwalimu Nyerere na Stesheni ya Kigoma imepewa jina la Mkapa.

Rais Samia amesema stesheni zingine zitapewa majina baadaye kadiri ujenzi wa reli ya SGR unavyoendelea.

Rais Samia ametoa majina hayo baada ya kuombwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kwamba wanaomba Stesheni Kuu ya SGR ya Dodoma ipewe jina Stesheni ya Samia.

Related Posts