CLIMATE CHANGE MARATHON kufanyika Pangani

Katika kuhakikisha jamii inakabiliana na mabadiliko ya tabianchi Shirika la TREE OF HOPE wameandaa Mbio za Marathon ya mabadiliko ya Tabianchi 2024 ( CLIMATE CHANGE MARATHON 2024) zitakazofanyika terehe 28 septemba 2024 wilayani Pangani Mkoa wa Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Wa Shirika Hilo Fortunata Manyelesa amesema lengo la Mbio hizo ni kukusanya Fedha na kuhamasisha watu kusaidia teknolojia ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Katika jamii ya Pangani na wamasai waliohamia Kijiji Cha MSOMERA wilaya ya Handeni wakitokea Ngororo.

“Marathon ya mabadiliko ya Tabianchi ni Mpango muhimu unaojibu changamoto kubwa za ukataji miti , uharibifu wa udongo, na uchaguzi wa hewa kwa jamii inayotegemea sana mkaa na Kuni kwa kupikia ” amesema Manyelesa

Mbio hizo za Marathon ya mabadiliko ya Tabianchi zinatarajia kunufaisha zaidi ya kaya 50000 Katika jamii ya za Pangani na Msomera huku ukilenga zaidi kupunguza uchaguzi wa hewa ndani ya nyumba , kuboresha afya na kuhifadhi rasilimali za asili pamoja na kuwawezesha wanawake na Vijana Kupitia mafunzo ya mbinu safi za kupikia, fursa za ujasiriamali na usimamizi endelevu teknolojia mpya.

Related Posts