Na Mwandishi wetu
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya kikazi mkoani Morogoro leo Agosti 02,2024, ambapo amezindua Hospitali ya Wilaya ya Gairo.
Pamoja na uzinduzi huo, amehutubia wananchi wa Wilaya ya Gairo walijitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Gairo.
Akizungumza na wananchi hao,Rais Samia amesema changamoto ya maji inakwenda kuondoka baada ya Serikali kutuo Sh. Bilioni 34 na tayari mikataba imeshasainiwa na kazi imeanza kuhakikisha wilaya hiyo inapata maji .