Nane zaliamsha Dar Kriketi ya Dunia U19

NCHI nane zimeliamsha jijini Dar es Salaam katika mashindano ya Kriketi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 19 barani Afrika, Tanzania ikiwa wenyeji.

Mashindano hayo yaliyozipanga timu hizo nne katika makundi mawili A na B yameanza jana kwenye viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam inatarajia kuchezwa kwa siku kumi hadi Agosti 11.

Mataifa yanayoshiriki ni pamoja na Tanzania, Ghana, Malawi, Sierra Leone, Nigeria, Msumbiji, Rwanda na Botswana. Timu hizi zitachuana kuwania nafasi tatu zinazowapa nafasi ya kwenda hatua inayofuata yatachezwa kwenye viwanja viwili Gymkhana na UDSM.

Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa habari wa Chama cha Kriketi Tanzania (TCA), Atif Saleem alisema Tanzania imejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo kama wenyeweji.

Alisema timu washindi wa kwanza kwenye kila kundi watafuzu kufuzu kwa divisheni ya kwanza na msindi wa pili kwenye kila kundi watacheza kusaka mshindi wa tatu ambaye atafuzu divisheni ya pili.

“Timu yetu iko katika hali nzuri na imejiandaa vilivyo kwa mashindano haya ambayo tunajivunia kuwa mwenyeji kwa ushirikiano na Baraza la Kimataifa la Kriketi (ICC),” alisema Saleem .

Kocha Msaidizi wa Tanzania ambaye pia ni mchezaji mkongwe Salum Jumbe alisema wako tayari kama taifa mwenyeji akieleza kuwa si vigumu kuwafundisha nyota chipukizi kwa sababu wana vipaji tayari.

“Tuna faida kubwa ya uwanja wa nyumbani, tuna matumaini kwamba wakati huu tutafanya vyema na kulifanya taifa letu lijivunie,” alieleza. Pia alisema lengo lao ni kufuzu kwa divisheni ya kwanza.

Related Posts