Mtanzania anayejizolea umaarufu kwa upambaji na kujishindia tuzo nchini Marekani

Baada ya safari ndefu akiyakimbiza mafanikio kutoka hapa Tanzania mpaka Marekani ambako alienda kutafuta maisha na akaanza kwa kubeba maboksi, Malkia wa Nguvu Doreen Fitzpatrick ambaye kwa sasa ni Mmiliki wa moja ya kampuni kubwa ya mapambo Washington Seattle Nchini Marekani iitwayo Sassyfly luxury event, amepata nafasi ya kuwania na kushinda Tuzo ya Muandaaji bora wa maua (best florist outside Seattle) inayotolewa na kampuni inayoshughulika na uandaaji wa harusi iitwayo Washington Wedding Day.

Akiongea baada ya kupokea tuzo hiyo Doreen amesema “Nilianza katika hali ngumu sana kwa sababu mara ya kwanza ninafanya mapambo ilikuwa kwenye harusi yangu mwenyewe baada ya kuona gharama zilivyokuwa kubwa na nilikuwa natamani kitu bora zaidi, kuanzia hapo sikuacha mpaka sasa kwa miaka mitano na nimekuwa nikiwania na kishinda tuzo hizi kubwa hapa kwenye Jimbo la Washington Nchini Marekani kwa miaka miwili mfululizo”

Mwaka jana 2023 Doreen alishinda tuzo ya Best Floral Designer of 2023
Na mwaka huu ameshinda Best Florist Outside Seattle ambapo amesema kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa sasa amefungua kampuni yake ya mpya ambayo inajihusisha ni ukodishaji wa vifaa vya mapambo ambayo itakuwa ikitoa asilimia kumi katika mapato itakayokuwa ikiyapata kwa ajili ya kuendeleza ndoto za Watoto wenye ndoto kubwa hapa nyumbani Tanzania.

“Baada ya mafanikio haya natamani kuwa baraka kwa wengine lakini Watoto wangu pia wajifunze kutoa hivyo kila asilimia kumi ya nitakachokuwa nakipata nitatoa kwa ajili ya kuwasaidia watoto walioko Tanzania wenye ndoto kubwa kuzifikia ndoto zao”

Doreen Mchaga kutoka Tanzania ambaye amekaa Marekani kwa miaka 10 mpaka sasa tangu mwaka 2014 ambapo alienda kutafuta maisha tu na alifikia kwa Mtu akampokea baada ya muda akamuacha akaanza kukaa pekee yake akibeba maboksi kupandisha kwenye magari kama kazi ya kumuingizia kipato hadi alipokutana na Mume wake, wakati wa harusi yake akawa anatafuta Mpambaji na kila aliyekuwa anakuja hakuwa anafurahia kile anakiona alikuwa anahitaji zaidi ndipo akaamua kupamba harusi yake mwenyewe na Watu wakapenda na wakawa wanauliza nani amefanya na alipowaambia ni yeye wakawa wanasifia na baadhi wakataka awafanyie mapambo na safari yake ikaanzia hapo.

Related Posts