Dawati la Elimu ya Usalama Barabarani yawafkia Waumini wa Ngarenaro.

Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani kupitia dawati la elimu ya usalama barabarani Mkoa wa Arusha limewaomba Waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kutoa elimu katika familia zao juu ya matumizi sahihi ya Barabara huku akiwakumbusha malezi bora na uangalizi wa Watoto.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa dawati la elimu ya usalama barabarani Mkoa wa Arusha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/Insp Rajabu Khatibu alipokuwa akitoa elimu na madhara ya kukiuka sheria za usalama barabarani katika msikiti wa AL Masjid Noor Ngarenaro ambapo amewaomba waumini wa dini hiyo kuendelea kutoa elimu kila wanapokutana katika familia na nyumba za ibada.

Ameongeza kuwa vijana wengi wamekuwa wakipoteza Maisha kwa sababu za kutoakufuata sheria za usalama Barabarani ambapo amewaomba waumini hao kukemea vitendo vya ulevi kwa baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakitumia vyombo vya moto huku wakiwa wamelewa.

Kwa upande wake Sajenti Athilio Choga kutoka dawati la elimu ya usalama barabarani Mkoa wa Arusha amebainisha kuwa lengo la dawati hilo ni kutoa elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa wa Pamoja katika matumizi sahihi ya Barabara ambapo amewakumbusha kauli mbiu ya mwaka huu katika wiki ya nenda kwa usalama Barabarani isemayo safari salama ufike salama.

Awali Shehe wa msikiti wa Ijumaa Ngarenaro Shehe Ramji amesema kuwa ni vyema waumini hao wafuate sheria ili kuepuka migongano na mamlaka zinazosimamia sheria hizo.

Related Posts