Serikali kupitia wizara ya Elimu sayansi na teknolojia imejipanga kufanya mapitio ya mitaala kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu ili kuwanoa wanafunzi watakaondana na ukuaji wa teknolojia ulimwenguni ili kuleta chachu kwa maslahi ya taifa ikiwa na lengo la kusimamia utekelezaji wa sera ya elimu ya 2024 itakayosaidia kuongeza ufanisi kwa watumishi wa Umma.
Akizungumza wakati akifungua mkutano wa 33 wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na teknolojia Prof. Carolyine Nombo amesema Wizara imejipanga kuhakikisha utekelezaji wa sera hiyo inaenda kuongeza kasi ya utekelezaji utakaondana na mabadiriko ya teknolojia Duniani.
Amesema Kwa Sasa Dunia inakua Kwa Kasi hivyo lazima kila mtu abadilike Kwa kuendana na Kasi ya tenkolojia ambayo Ili kuongeza ufanisi
Kwa upande wake Bi Honesta Ngoli Afisa elimu kazi mwandamizi kutoka ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na watu wenye ulemavu idara ya kazi amesema wamejipanga kuwanoa vijana watakao endana na kasi ya teknolijia huku ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono rais a jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kuleta maendeleo nchini
Aidha Mwenyekiti wa TUGHE tawi la wizara ya elimu, sayansi na teknolojia amesema baraza hilo limekuwa muhimili katika suala la elimu ikiwemo kutetea maslahi ya wananchi pamoja na kutatua changamoto baina ya TUGHE na CWT na kuungana ili kufanyakazi kwa kushirikiana.