Rais Samia mgeni rasmi uwekaji wa jiwe la msingi upanuzi kiwanda cha sukari Kilombero K4

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uwekaji Jiwe la msing la upanuzi Kiwanda cha sukari cha kilombero-K4 ambao utafanyika Agosti, 4 2024.

Akizungumza leo Agosti 2, 2024 na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Derick Stanley amesema katika mkakati wa kuungana juhudi za serikali kuhakikisha nchi inakua inakua na utoshelevu wa bidhaa ya sukari.

Alisema upanuzi wa mradi huo gharama yake itakuwa Sh bilioni 744 na unakamilika Juni mwaka 2025.

“Kukamilika kwa mradi huu kutaongeza uwezo wa kampuni hii1 kuzalisha sukari kutoka tani126,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 271,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025,”alisema Stanley.

Alisema kiwanda hicho cha K4 kilianza kujengwa miaka miwili iliyopita ni kiwanda cha kisasa kinaongoza kwa ukubwa Africa Mashariki.

Aliongeza kuwa kukamilika kwa kiwanda hicho kitapunguza changamoto za uhaba wa sukari nchini na kusaidia serikali kutokuagiza sukari nje ya nchi.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano na Mahusiano kwa Wadau wa kiwanda hicho, Victor Byemwelwa alisema amewahimiza wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa za mradi huo.

Related Posts