KLABU ZA ROTARY NCHINI ZIMEENDESHA ZOEZI LA VIPIMO NA UCHUNGUZI WA KITABIBU BURE

KLABU za Rotary nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Vilabu Vya Rotary Vya Oysterbay, Sunset, na Ukonga wameendesha zoezi la Siku ya Afya ya Familia ya Rotary (RFHD) nchini Tanzania kwa kufanya uchunguzi na vipimo vya Afya bure kwa wakazi wa Shule ya Mzambarauni Kata ya Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Rotary Tanzania Sophia Chamzingo amesema “Rotary Tanzania, kwa kushirikiana hasa na Klabu ya Rotary ya Oysterbay, imekuwa ikiandaa kambi za matibabu kwa kushirikiana na Klabu ya Rotaract ya Kairiuki tangu mwaka 2012 lengo likiwa kutoa huduma za afya msingi kwa jamii ya Dar es Salaam.

Aidha Chamzingo amesema Kampeni ya afya ya leo inaadhimisha hatua muhimu sana, ikiwa imeongezeka mara tatu ukubwa wa kambi za matibabu zilizofanywa hapo awali na klabu yetu.

Pia amesema Jumla ya Wakazi 5000 kutoka Ukonga na Maeneo ya jirani wamepatiwa huduma za Afya na Elimu bila malipo “.

Matibabu hayo yamefanyika kwa ushirikiano mkubwa wa timu ya wahudumu takribani 100 wakiwemo madaktari wa kawaida 50 na wataalamu wengine 50 wa meno,macho,ngozi,watoto na huduma nyingine.

Pia Klabu Mbalimbali zimeweza kufanikisha tukio hilo ikiwemo Klabu ya Rotary Kairuki, Muhimbili, KIUT,Alpha na E-Swahili.

Sanjari na hilo Kampuni mbalimbali zimeungana na Klabu za Rotary kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kuwashukuru sana Vilabu vya Rotary na Rotaract washirika wetu, vilevile washirika muhimu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Awamu ya Sita Ikiongozwa na Raisi Doctor Mama Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Afya,Bill& Melinda Gates Foundation, , MDH, Ocean Road Cancer Institute,

Light of the World, CCBRT, Tanzania Dental Association, Local Government Regional

Medical Team ,Ministry of Health, EngenderHealth , Rotary Club of Ukonga, Rotary Club

of Sunset, Rotaract Clubs of KIUT, Kairuki, Alpha, Muhimbili and e-Swahili, Sayona Drinks

Tanzania, SGA Security, Guaranty Bank, White sands Hotel , Medinova Specialized

Polyclinic ,SBC Pepsi, NV Pharmaceuticals, Friends of Rotary, Rotarians, Primary Schools

of Ukonga, Juhudi, Jica and Amani, Leadership of Mzambarauni Primary School, Rotary

Family Health Days (RFHD) ,Rotary Club of Oyster Bay ,Afya Intelligence, Tarmal Industries,

Hitech Sai na Chemicotex pamoja na Bakhresa food.”



Related Posts