Waziri Silaa avunja bodi ya TTCL

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amevunja bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) baada ya mwenyekiti wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Julai 23, 2024.

Bodi hiyo imevunjwa jana Agosti 2, 2024 na waziri huyo kutokana na mamlaka aliyonayo.

Taarifa ya kuvunjwa bodi hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano wa wizara hiyo, Isabela Katondo.

Rais Samia alitengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTCL, Zuhura Muro na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga.

Viongozi wengine ambao walitenguliwa siku hiyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, Brigedia Jenerali mstaafu, Yohana Mabongo na Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Maharage Chande.

Pia, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Profesa John Nkoma na Ofisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Justina Mashiba.

Related Posts