Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Mashabiki wa klabu ya Simba wote kwa kufanikisha Tamasha la Simba Day mwaka 2024.
Rais Samia ameongea na Wanasimba moja kwa moja baada ya kumpigia simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa akiwa ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Hongereni sana Wanasimba kwa Tamasha bora la Simba Day. Mwaka jana tulikuwa wote lakini leo imeshindikana kutokana na ratiba kuwa ngumu nimeshindwa kuwa hapo”
“Nafahamu msimu uliopita hamkuwa bora sana lakini yaliyopita si ndwele, nyanyukeni songeni mbele,” amesema Dkt. Samia