Kiungo Mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba, Joshua Mutale amepokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Simba baada ya utambulisho huku akiibuka na jezi namba 7 ambayo ilikuwa inavaliwa na Willy Onana.
Onana anatajwa kuuzwa na Simba Uarabuni kwa dola 100,000 na katika utambulisho wa kikosi cha Simba cha msimu wa 2024/25 jina lake halipo hivyo ni rasmi sio sehemu ya kikosi cha klabu hiyo msimu ujao.
Mutale amepewa namba ambayo alikuwa anaitumia kabla ya kujiunga na Simba akiwa na klabu ya Power Dynamos ya Zambia.