Elizaberth Msagula Lindi,
Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC limeunganishia gesi zaidi ya nyumba 1500 katika Mikoa ya Dar es Salam,Lindi na Mtwara ikiwa ni katika kutekeleza mkakati wa Taifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia wa mwaka 2024-2034.
Mkakati huo unalenga hadi kufikia mwaka 2034 wananchi wanaotumia nishati safi yakupikia wawe wamefikia asilimia 80.
Afisa maendeleo kutoka TPDC Ali Mluge akiwa katika viwanja vya nane nane Kanda ya kusini yanayofanyika eneo la Ngogo amesema wanaendelea kutoa elimu kupitia kitengo cha mawasiliano ili wananchi waone umuhimu wa kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa waanze kitumia gesi na kwamba kadiri siku zinavyokwenda wanaona mabadiliko yenye mwamko mkubwa katika matumizi ya nishati hiyo ya gesi inayosaidia kuokoa afya za watu na mazingira.
Aidha amesema kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 watatekeleza mradi wakuongeza nyumba zingine kuunganishia gesi nyumba 451 kwa Mkoa wa Lindi na Mkuranga nyumba 500,mradi ambao tayari upo katila hatua mbalimbali za utekelezaji kwani tayari ameshapatikana akisema kwa sasa serikali imewekeza fedha nyingi kila mwaka yakuongeza mtandao wa mabomba ili kuwafikia watu wengi zaidia ambapo kwa sasa anapata huduma hiyo bila kulipia gharama yeyote.
Mlunge pia amesema kwa sasa TPDC inaongeza kasi ya kufungua vituo vya kijazia gesi kwenye magari ambavyo wameanza kwa Mkoa wa Dar es Salam lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa nishati hiyo.