UTANI WA SIMBA NA YANGA UMEKWENDA KWENYE MAFANIKIO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Michezo,siangalii Simba tu naiangalia Tanzania,amekuja kiongozi wa Soka kutoka Uganda ameshanga ule umati wa Watu,nikamwambia ukija na kesho (leo Yanga Day) atakutana na umati mkubwa mwengine, hii ndio Tanzania.

 

 

“Simba na Yanga ndio alama za mpira wa Taifa hili kama Waziri nimefurahi hicho kinachondelea kufanyika na vilabu vyetu,Mafanikio kwenye klabu ndio chanzo cha kufanya vizuri. Na ninachofurahi zaidi pia kwa sasa Simba na Yanga wanashindania mambo ya maana, Simba anashindania sana michuano ya Afrika ”

 

 

“Halikadhalika na Yanga nae hivyo hivyo ,Simba walianzisha Simba Day na Yanga nae yumo kwenye Yanga Day, hayo ndio mafanikio utani wao sasa umekwenda kwenye mafanikio” Mhe. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni Sana na Michezo.

Related Posts