UNAWEZA kusema mtoto wa nyoka hazai kuku, kwani mtoto wa aliyekuwa Mfadhili na Mwenyekiti wa Yanga, Mehboub Manji ametua Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia Tamasha la Wiki ya Mwananchi.
Mehboub ametua uwanjani hapo kimyakimya katika tamasha hilo la sita la Yanga ikiwa ni mara ya kwanza tangu baba yake alipofariki dunia Juni 29, akiwa Marekani.
Mara baada ya kuwasili Mehboub alipokelewa na maafisa wa Yanga na kupelekwa Jukwaa la watu mashuhuri.
Inaelezwa kwamba Mehboub amepewa mualiko maalum na uongozi wa Yanga, ambao unataka kutambua mambo makubwa aliyofanya baba yake wakati wa enzi za uhai wake.
Mbali na kumwakilisha baba yake Mehboub pia ni shabiki wa Yanga akiwahi kukiri kwamba wamerithi kwa mzazi wake huyo.