MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango, amehudhuria kilele cha tamasha la ‘Wiki ya Mwananchi’, akiwa ndiye mgeni rasmi na kuipongeza Yanga kwa kufunika kwa tamasha hilo la Wiki ya Mwananchi.
Wakati wa utambulisho wa wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, washereheshaji wa tamasha hilo, Zembwela na Maulid Kitenge walimtangaza Mpango kuwa mgeni rasmi kabla ya baadae hajashuka uwanjani kuzungumza na mashabiki akiwa na msafara wa vigogo wengine wa serikali kabla ya kutaka wananchi kupokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuzungumza kwa njia ya simu.
Mpango na mkewe Mama, Mbonimpaye, walisafiri asubuhi hii ya Agosti 4, wakitokea Dodoma kuja Dar es Salaam kwa usafiri wa treni ya kisasa ya umeme inayotumia reli ya SGR.
Tamasha hilo la sita kufanyika tangu mwaka 2019, liliasisiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mshindo Msolla.