UTAMBULISHO wa mchezaji mpya wa Yanga, Clatous Chota Chama, umeibua shangwe la mashabiki wa timu hiyo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Chama amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Simba aliyoitumikia kwa misimu sita tofauti tangu alipojiunga nayo Julai Mosi, 2018, akitoka Klabu ya Lusaka Dynamos ya kwao Zambia.
Usajili wa nyota huyo ulizua gumzo nchini kutokana na mashabiki wengi kutoamini kama mchezaji huyo angeondoka na kujiunga na Yanga ingawa Mwanaspoti lilikuwa mstari wa mbele kuandika ukweli juu ya sakata hilo.
Mbali na Chama, ila wachezaji wengine walioteka hisia za mashabiki ni Prince Dube aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Azam FC, Pacome Zouzoua na Stephane Aziz KI.