WAKATI utambulisho wa wachezaji ukiendelea, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango wasitisha zoezi hilo na kuzungumza na wananchi.
Hayo yalitokea baada ya tukio la utambusho kusitishwa na kumkaribisha Makamu wa Rais ili aweze kusema neno ambapo alimpigia simu Mh. Rais Samia ili aweze kutoa neno kwa Wanajangwani kama ilivyokuwa desturi yake.
Rais. alisema kuwa; ”Nawapongeza Yanga na hongereni kwa kusajili vyuma msimu huu, ninajua mmejipanga vizuri.”
Aidha Dkt. Mpango alisema; “Nawapongeza viongozi wa klabu na benchi la ufindi la Yanga kwa vifaa vilivyoshuShwa ‘watatweza kweli’.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumza na mashabiki wa Yanga, ikumbukwe kuwa Mwaka Jana alikuwa Mgeni Rasmi wa siku ya Wananchi.
Hata hivyo siku ya jana Rais Samia alizungumza na mashabiki wa Simba katika siku yao kwa njia ya simu.
Mara baada ya Rais kumaliza kuzungumza, Katibu wa Wizara wa Utamaduni, Sanaa na Michezo aliutangazia umma kwamba kwa msimu huu Goli la Mama linaanzia hatua ya awali kwa wawakilishi wa nchini, Yanga, Simba, Azam FC na Coastal Union kwa kila bao la mechi ya ushindi ni Sh 5 Milioni, huku hatua ya Robo fainali ikiwa ni Sh 10 Milioni na ile ya Nusu fainali itakuwa ni Sh 20 Milioni na kufika fainali itatangazwa baadae.
Yanga na Azam FC zitacheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba na Coastal zitashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga, Azam na Coastal zenyewe zitaanzia raundi ya kwanza wakati SImba ikicheza raundi ya pili. Mechi za awali zitapigwa kati ya Agosti 16-25.