Hamis Mabetto sasa ni Mwananchi

MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ‘Bugatti’ amesema amemsilimisha rasmi Mwanamitindo maarufu nchini, Hamisa Mobetto kuwa shabiki wa timu hiyo ya Jangwani kutoka Msimbazi.

Hatua hiyo imejiri wakati wa tamasha la kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ ambapo msanii huyo alivalishwa jezi ya Mwananchi na Stephane Aziz KI aliyeitwa jukwaani na Haji Manara.

Katika tukio hilo, Manara amesema, amemsalimisha rasmi msanii huyo na kumvalisha jezi ya Yanga huku Mobetto akionekana mwenye furaha usoni mwake.

Hata hivyo, inaelezwa ushawishi mkubwa wa msanii huyo umetokana na ukaribu wa mchezaji wa Yanga, Stephane Aziz KI ambaye mara kwa mara amekuwa naye katika matukio mbalimbali.

Mobetto ambaye anajulikana ni shabiki mkubwa wa Simba, licha ya kuvaa jezi hiyo ila hakuzungumza chochote kama kweli ameachana nayo na kujiunga na Yanga.

Awali Hamisa alikaririwa na Mwanaspoti kwamba yupo karibu na Aziz KI, lakini bado ni Mnyama, lakini kwa kilichotokea jana kimemaliza utata mbele ya mashabiki wa klabu hiyo.

Related Posts