“Hii ndio Yanga Ndugu Waandishi wa Habari, leo ni siku ya raha tumeenjoy….. Watu tuna makausha damu, Watu tunadaiwa mikopo hata hela ya kunywa bia hatuna lakini Yanga inakusuuza”
“Yanga sasa hivi imekuwa raha raha raha sana, tarehe 8 Simba akitufunga wachukue panga walinoe kwenye lami wanikate mguu utoke kabisa wauinue juu waseme huu ni ubaya ubwela” maneno ya Shabiki wa klabu ya Yanga, maarufu kama Shetani wa Yanga.
Shabiki huyo alitoa maneno haya jana Agosti 4 baada ya klabu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows FC katika mchezo wa kirafiki katika kilele cha Wiki ya Wananchi.
Mechi inayofata ni ya watani wa Jadi Simba na Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 08, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya Saa 10:00 Jioni.
Huku matajiri wa Jiji Azam FC wakivaana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya Ngao ya Jamii katika Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar majira ya Saa 1:00 Usiku.