ELIMU ITOLEWE KUHUSU BIASHARA YA KABONI NCHINI -; DKT. DUGANGE – MWANAHARAKATI MZALENDO

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI (Afya) Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa wito kuwa elimu ya Biashara ya Kaboni itolewe sababu kuna fursa kwa Halmashauri nyingi kunufaika na biashara hiyo nchini.

Dkt. Dugange amesema hayo alipotembelea Banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nanenane, Nzuguni mkoani Dodoma, Agosti 4,2024.

Amesema elimu itolewe kuhusu Biashara ya Kaboni na jinsi Halmashauri zinavyoweza kunufaika nayo sababu Halmashauri nyingi nchini zinaonekana hazina uelewa wa fursa zilizopo katika Biashara ya Kaboni na faida yake.

“Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) kijitangaze zaidi ili kiweze kufahamika zaidi na kufikia wadau wengi.

“Ni muhimu pia kituo hiki kufungua Ofisi za Kanda ili kuimarisha uwepo wake na kuhakikisha huduma zake zinawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Pia, Dkt. Dugange ameongeza kuwa Halmashauri zitenge bajeti maalum kwa ajili ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira na kuhakikisha miti inapandwa na kutunzwa ipasavyo, na ni muhimu Halmashauri zizingatie hili katika mipango yao.

#KonceptTvUpdates

Related Posts