MR. MANGURUWE ATUNUKIWA UDAKTARI, SASA AWA DR. MANGURUWE! – MWANAHARAKATI MZALENDO

#BIASHARA Mwanzilishi na mmiliki wa Mradi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mnkondya (maarufu kama Mr Manguruwe) wa Zamahero Dodoma nchini Tanzania ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Mitandaoni kupitia mradi huo, ameutunukiwa Shahada ya Udhamiri wa Falsafa ya Biashara na Maendeleo ya Jamii ( Doctor In Business and Humanity) ya Chuo kikuu cha Afican Graduate University.

Ametukuniwa udaktari huo baada ya kuongoza vizuri biashara zake, kusaidia wengine na kuwa na Falsafa ya Kuamini na Kufanya Kazi kwa Juhudi na Maarifa ili Kufikia Malengo Makubwa na Kufundisha na Kuhamasisha Wengine kwa Maendeleo ya Nchi”.

Digrii hiyo ya Udhamiri imetolewa na Professor Stephen Nzowa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo wawekezaji katika mradi wake, ndugu, Jamaa na Marafiki zake kutoka ndani na nje ya nchi.

Mr. Manguruwe kwa sasa Dr. Manguruwe ameeleza furaha yake baada ya kutunukia udaktari huo, amemshukuru Mwenyezi Mungu na Mke wake Rose Simon Mnkondya kwa kuwa naye bega kwa bega ili kutimiza kazi zake vizuri na kuweza kutunukiwa Udaktari wa Falsafa ya Biashara na Maendeleo ya Jamii.

Cc; Malunde

#KonceptTvUpdates

Related Posts