MOYO WA BINADAMU KUFUNGUA LOCK ZA iPHONE – MWANAHARAKATI MZALENDO

Katika hatua mpya ya ubunifu, kampuni ya Apple inatarajia kuanzisha teknolojia ambayo itaruhusu watumiaji kufungua simu zao za iPhone kwa kutumia mapigo ya moyo, badala ya alama za vidole au utambuzi wa uso.

Habari mpya kutoka Mtandao wa Wealth zinaeleza kuwa teknolojia hii itatumia utendaji wa kitu kinachoitwa ECG, ambacho tayari kinapatikana kwenye saa za mkononi za Apple. Kitu hiki kinachotumia data ya mdundo wa moyo kwa ajili ya kupima mapigo ya moyo na matumizi mengine ya kiafya, sasa kitapanuliwa ili kuunganishwa na teknolojia ya kufungua simu.

Taarifa kutoka kwa Wealth zinaeleza kwamba iPhone mpya itakuwa na uwezo wa kuchukua mapigo ya moyo ya mtumiaji kwa jinsi anavyoishikilia simu yake, hivyo kuweza kutambua na kufungua simu hiyo kwa usahihi. Hii inaashiria hatua kubwa katika maendeleo ya teknolojia ya usalama na urahisi wa matumizi, ambapo Apple inaendelea kuongoza kwa ubunifu katika tasnia ya vifaa vya kielektroniki.

Kwa sasa, kampuni inatarajia kwamba teknolojia hii itachangia katika kuboresha uzoefu wa mtumiaji kwa njia mpya na ya kipekee, na kuongeza usalama na faragha kwa watumiaji wa vifaa vya Apple.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts