WANANCHI wakipatiwa elimu ya wazalishaji kutumia Viwango katika mnyororo mzima wa uzalishaji kuanzia mashambani, matumizi ya pembejeo bora na uhifadhi wa mazao unaozingatia Viwango.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MENEJA wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kati Bw. Nickonia Mwambene, amesema katika maonesho ya Nanenane mwaka huu wanatilia mkazo elimu ya wazalishaji kutumia Viwango katika mnyororo mzima wa uzalishaji kuanzia mashambani, matumizi ya pembejeo bora na uhifadhi wa mazao unaozingatia Viwango.
Mwambene ameyabainisha hayo leo Agosti 5,2024 wakati akizungumza na wandishi wa habari katika banda la TBS katika maonesho hayo yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo ameongeza kuwa bidhaa salama ni kichocheo cha uchumi wa nchi.
“Kwasababu inakubalika kwa watumiaji, ni rahisi kupata soko la ndani na nje ya nchi, ni rahisi kuvuka katika mipaka ya kiforodha, ni rahisi kushindana sawia katika sokk, kuondoa madhara kwa watumiaji”, amesema.
Ameongeza kuwa Serikali inawekeza kuwapa elimu bure kupitia TBS ili wakidhi ubora na kuwanyanyua ili wakue na kushindana katika soko la bidhaa zinazofanana zilizo katika soko lao.
“Kwa kuwa na katika maonesho haya wote tunatambua kuwa kilimo ni biashara hivyo kwa kutumia taratibu za kilimo bora, Tanzania itapata bidhaa bora katika soko ambazo zitashindana na bidhaa zanazotoka nje ya nchi “, ameongeza.
Amesema Serikali kupitia TBS mkazo mchango wa wajasiriamli na Kwasababu hiyo Shirika hilo linawalea kwa karibu katika kuwapa elimu bure na kufanya ukaguzi bure ili wakidhi viwango vya ubora na waweze kupeleka bidhaa zao sokoni na kushindana na zile zinazotoka nje ya Nchi.
MENEJA wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kati Bw. Nickonia Mwambene,akizungumza na waandishi wa habari katika banda la TBS wakati wa maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma
WANANCHI mbalimbali wakiendelea kupatiwa elimu ya wazalishaji kutumia Viwango katika mnyororo mzima wa uzalishaji kuanzia mashambani, matumizi ya pembejeo bora na uhifadhi wa mazao unaozingatia Viwango.