MNEC ASAS amteua Jasmine Ng’umbi kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi za CCM wilaya ya Mufindi.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Salim Abri Asas amemteua Jasmine Ng’umbi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za CCM wilayani Mufindi.

Uteuzi huu umefanyika baada ya MNEC Asas kutembelea ujenzi unaoendelea wa ofisi ya CCM katika kata ya Upendo, wilaya ya Mufindi, ambapo Jasmine Ng’umbi alifanya changizo la fedha ili kusaidia kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo.

Akiongea mbele ya MNEC, Jasmine Ng’umbi amemuomba msaada wa kumalizia ujenzi wa ofisi hiyo, akieleza kuwa ofisi hiyo itasaidia kutatua changamoto za wana CCM na wananchi kwa ujumla huku akimshukuru MNEC Asas kwa kutembelea ujenzi huo.

Kwa upande wake, MNEC Asas ameahidi kumalizia ujenzi wa ofisi hiyo na kumteua Jasmine Ng’umbi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za CCM wilayani Mufindi.

Amemtaka binti huyo kufanya tathmini ya ofisi zote za CCM wilayani Mufindi ambazo zimefikia hatua ya kumaliza ujenzi ili ziweze kumaliziwa.

MNEC Asas pia amesisitiza umuhimu wa kujitolea kwa wanachama katika maendeleo ya chama, akisema CCM itajengwa na wanachama wenyewe.

Ziara ya MNEC Asas ya kukutana na Halmashauri kuu za CCM za wilaya Mkoani Iringa inaendelea na tayari ametembelea wilaya ya Mufindi na Kilolo akitarajiwa kufika wilaya ya Iringa vijijini na wilaya ya Iringa Mjini.

Related Posts