Teknolojia ya uhimilishaji kutoka Marekani na Brazil kuleta mapinduzi sekta ya mifugo

Wafugaji wazawa sasa wanaweza kuongeza uzalishajiwao wa maziwa na nyama kufuatia kufikiwa na teknalojia mpya na ya kisasa ya uhimilishaji ambayo imefanyiwa utafiti wa kina kutoka nchini Marekani naBrazil.

Teknalojia hiyo mpya inayohusisha kuchanganya mbegu za ng’ombe wa asili na mbegu za kutoka Marekani na Brazil ambapo hupelekea kupatikana kwang’ombe chotara imeletwa hapa nchini na kampuni yaURUS inayojihusisha na usambazaji wa mbegu bora za ng’ombe wa nyama na maziwa duniani

Akiongea katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, meneja mkazi wa URUS Tanzania Edson Mfuru alisema ng’ombe wanaozalishwa kupitia uhimilishaji wanaoufanya wanauwezo mkubwa wa kuzalisha maziwa na nyamaukilinganisha na mbegu za asili.

Pamoja na kwamba Tanzania ni nchi ya pili kwa wingiwa mifugo barani Afrika baada ya Ethiopia, mchangowa sekta hii kwa pato la taifa bado ni mdogo. Sababuzinazotajwa kupelekea mchango mdogo ni pamoja namatumizi ya mbegu za asili ambazo zinatoa uzalishajimdogo.

Meneja mkazi huyo anasema wakati mbegu za asilizikitoa maziwa kati ya lita 1-5 kwa siku, ng’ombechotara ambao huzalishwa kwa kutumia mbeguwanazotoa Brazil na Marekani huzalisha kati ya lita15-25 kwa siku hivyo kumhakikishia faida mfugaji.

Kwa upande wa nyama anasema mbegu za asilizinauwezo wa kutoa kiwango cha juu kabisa cha nyama kilo 200 wakati ng’ombe chotara wanaotokanana mbegu zao huweza kutoa hadi kilo 1,000

Uhimilishaji ambao hupelekea kupatikana kwang’ombe chotara kama Girolando, hufanyika ilikubadilisha chakula kuwa misuli kwa ufanisi zaidi. Chakula kidogo huitajika kwa ajili ya kuzalisha kiasikikubwa zaidi cha maziwa au nyama. Matumizi yachakula kidogo kulisha ng’ombe husaidia kupunguzagharama za ulishaji ambazo huwa kubwa katikaufugaji,”

Mfuru alisema kwa sasa URUS Tanzania inafanya kazina wafugaji katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Iringa, Njombe, Mbeya na Kagera, ikiwapaelimu juu ya mbegu bora na pia kuwapatia mbeguzilizoboreshwa katika maeneo yao.

Ingawa kwa sasa tunapatikana katika maeneo niliyoyataja, lengo letu ni kuwafikia wafugaji popote walipo hapaTanzania. Madhumuni yetu ni kuhakikisha kila mfugajianafikiwa popote pale alipo na kupatiwa hudumazitakazomsadia kuboresha ufugaji wake. Tunaendeleakujitanua na kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji yawafugaji wote,” aliongeza.

Related Posts