Watano wahofiwa kufa maji wakitoka ‘Siku ya Mwananchi’

Buchosa.Watu watano wamehofiwa kufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafirua  kuzama ndani ya ziwa Victoria walikuwa wakitoka kisiwa cha Yozu kilichopo Kata ya Bulyaheke Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza walipokwenda kwenye kilele cha Yanga day.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga amethibitisha kutokea kwa tukio ambalo limetokea usiku Agost 5 ,2024   majira ya saa mbili usiku.

Amesema mtumbwi huo ulikuwa umebabe  mashaki 23 wa Yanga ambao wanatoka  tawi la Yanga Kijiji cha Mbungani Kata ya Bulyaheke.

Amesema hadi sasa mwili wa mtu moja umepatikana huku wakiendelea kutafuta miili mingine miwengi vyombo vya ulinzi na usalama vimepiga Kambi huko wakishirikiana na wananchi kutafuta watu waliozama ambao hawajapatikana.

Mwenyekiti wa maafa Kisiwa cha Yozu Juma Limbe amesema mashaki wa Yanga tawi la mbungani na tawi la Yozo huwa wanatembeleana mara kwa mara  kama ndugu lakini ajali liyotokea jana imewasikitisha.

Endelea kufuatia mitandao ya Mwanaspoti kupata habari zaidi.

Related Posts