Polisi wahoji maswali 2 watuhumiwa ubakaji wakidakwa

 

WAKATI Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa msichana anayedaiwa mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi limeitaka jamii kutoendelea kumtonesha binti huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Licha ya kwamba Masauni hakufafanua kwa kina kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi katika taarifa yake leo Jumanne limesema uchunguzi unaendelea vizuri na wananchi waendelee kuwa nasubira kwani taarifa itatolewa baada ya kukamilisha yale ambayo sheria za nchi zinavyoelekeza.

Kupitia Msemaji wake, DCP – David Misime amesema “Jeshi la Polisi linatoa wito sote kwa pamoja tuendelee kutafakari namna tunavyoendelea kujadili jambo hili na tunavyotoa maoni kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari je hatuendelei kumtonesha huyu binti majeraha aliyonayo moyoni? Je kwa kuendeleza hayo familia yake hatuendelei kuijeruhi kisaikolojia?

“Pia tunaendelea kusisitiza mwenye taarifa ya ziada atuwasilishie kwa njia iliyosahihi kwa kutumia mifumo iliyopo bila kuendelea kumuumiza,” amesema Misime

Tarehe 4 Agosti mwaka huu zilisambaa video katika mitandao ya kijamii zikiwaonesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu.

Pia katika video hiyo binti huyo alisikika akielekeza anakotokea na kumwomba msamaha mtu aliyetambulishwa kwa jina la afande.

About The Author

Related Posts