TAMISEMI YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA TAKIMWU

Na Angela Msimbira, OR-TAMISEMI

OFISI ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa imezindua Mpango Mkakati wa Takwimu na utekelezaji wake ambao umelenga kuwezesha upatikanaji, ufikiaji na matumizi ya takwimu katika ngazi ya mamlaka za serikali za mitaa.

Akizungumza wakati wa kuzindua mkakati huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Adolf Ndunguru amesema matumizi hafifu ya teknnolojia katika ukusanyaji wa takwimu hasa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa unachangia katika kukosekana kwa takwimu sahihi na zenye ubora ambazo ni muhimu katika kufanya maamuzi mbalimbali.

Amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha uwezo wa watendaji wa serikali katika ukusanyaji, uchambuzi na matumizi ya takwimu ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Ndunguru anafafanua kuwa kuanzishwa kwa mpango hui ni hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa usimamizi wa takwimu nchini kutokana na uwepo wa mahitaji ya takwimu kwa kiwango cha juu.

Pia ni kutokana na uwepo wa matumizi hafifu ya takwimu katika kupanga mipango kwenye maeneo mbalimbali, mpango huu utasaidia kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

Amesema pia uwepo wa mpango huo utasaidia kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika mipango mbalimbali ya maendeleo na kuunga mkono mpango wa kitaifa wa takwimu.

Aidha, Ndunguru ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau, serikali mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafasi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango mkakati huo.

“Ushiriki wenu ni muhimu katika kuhakikisha tunapata tawkimu sahihi zenye ubora na zinaoweza kutumika katika maamuzi yetu.”amesisitiza Ndunguru

Amesema kila mdau ana jukumu katika kuhakikisha mfumo wa takwimu unafanyakazi kwa ufanizi na unatoa matokeo chanya kwa wananchi kwani bila takwimu sahihi zenye ubora mipango haitakuwa na uhalisia,

Akitoa salama Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Dk JohnMboya amesema mkakati huo ni muhimu kwani unaenda kuleta uwazi na uwajaibikaji kwenye halmashauri ambazo ndizo zinachangia kwa kiasi kikubwa takwimu za nchi.

Pia ametumia fursa hiyo kuiomba Ofisi ya Rais –TAMISEMI kuangalia namana ya kuendelea kuwajengea uwezo watakiwmu katika ngazi ya halmashauri ili waweze kusimamia vizuri.

Pia ameomba waratibu katika ngazi za halmashauri na mikoa kupatiwa vitendea kazi na kushauri uwepo wa jukwaa la kidigitali la takwimu ambalo litawezesha upatikanaji wa takwimu.

Related Posts