Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Namibia Mhe. Nangolo Mbumba ambaye yuko Nchini Tanzania kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Samia Suluhu Hassan jana 25.04.2024 alitembelea Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambao ni waagizaji na wasambazaji halali wa Bia za Windhoek nchini Tanzania.
Akiwa Ofisi za Mabibo Mhe. Mbumba
alimshukuru Mama Benedicta Rugemalira (mmiliki wa kampuni hiyo) kwakua na mahusiano mazuri na Namibia Breweries Ltd (NBL). Pia Mh. amewataka watanzania kuchangamkia fursa zilizoko nchini mwake.
Naye mmiliki wa Kampuni ya Mabibo amemhakikishia Mh. Rais kuwa ataendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Mabibo na NBL ambao umedumu kwa miaka 18 sasa. Pia kuendelea kutafuta wawekezaji wengine kuja kuwekeza Tanzania.
Picha mbalimbali za Rais wa Namibia The.Nangolo Mbumba akiwa na Timu ya Ofisi ya Kampuni ya Mabibo.
Rais wa Namibia Mhe. Nangolo Mbumba akiwa anatembelea ofisi za Mabibo ambaye yuko mwaliko wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.