Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ameshuhudia utiaji saini wa mikataba 24 baina ya TARURA na Wakandarasi yenye thamani ya shilingi Bilioni 9.6.
Katika hafla hiyo Mhe. Shigela amewataka wakandarasi hao kukamilisha miradi yao mapema na kwa viwango vyenye ubora ili kuendelea kutengeneza uaminifu kwa serikali na hivyo kupewa kazi nyingine.
Naye,Meneja wa TARURA Mkoa wa Geita Mhandisi David Msechu amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi bilioni 20.3 zimeidhinishwa na serikali kwa ajili ya ujenzi,ukarabati na matengenezo ya barabara mkoani humo.