BAADA ya Mchenga Star kuifunga Pazi kwa pointi 65-62 katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, kocha wa timu hiyo, Mohamed Yusuph amesema haikuwa raisi kwa timu yake kuishinda timu hiyo.
Yusuph ameliambia Mwanaspoti kuwa Pazi ilionyesha kiwango bora katika robo zote nne.
Alisema ushindi walioupata katika mchezo huo ulitokana na nidhamu ya wachezaji pamoja na kujituma.
“Kwa kweli nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyoifanya katika mchezo huo uliokuwa ni mgumu” alisema Yusuph
Baadaye nyota wa timu hiyo Amin Mkosa, alisema ushindi wao umewanyooshea njia ya kucheza hatua ya nane bora.
Katika mchezo mwingine UDSM Outsiders iliifunga timu ya Crows kwa pointi 72-42.