SERIKALI KUANDAA UTARATIBU WA KUTAMBUA MCHANGO WA VIJANA WANAOJITOLEA – NAIBU WAZIRI SANGU

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza leo na wananchi wa Kata ya Kalambanzite, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Sehemu ya wananchi wa Kata ya Kalambanzite, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa  wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu mara baada ya kuwasili katika Kata hiyo, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kalambanzite wakimlaki Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu mara baada ya kuwasili katika Kata hiyo ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu  akisalimiana na baadhi ya  wananchi mara baada ya kuwasili katika  Kata ya Kalambanzite , Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, ikiwa ni ziara yake ya kwanza  tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo.

Na. Lusungu Helela-Rukwa

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu amesema Serikali inaandaa utaratibu rasmi wa kutambua mchango wa vijana wanaojitolea kwenye Taasisi mbalimbali za Serikali huku akiwataka vijana  hao kuwa wavumilivu na  wasikatishwe tamaa.

Amesema utaratibu huo utasaidia kupata watu sahihi wanaojitolea badala ya kupata mamluki ambao hupenyezwa na ndugu zao pindi fursa za ajira zinapojitokeza.

Mhe. Sangu ametoa kauli  hiyo leo kwa nyakati tofauti  wakati akizungumza  katika mkutano ya hadhara uliofanyika katika Kata ya Ikozi na Kalambanzite zilizopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Mkoani Rukwa, ikiwa ni ziara yake ya  kwanza tangu alipouteliwa kushika  wadhifa huo.

 Amesema udanganyifu huo umekuwa ukifanywa na  baadhi ya Watumishi wasio waaminifu wenye ndugu zao na kupelekea  manung’uniko kwa vijana sahihi wanaojitolea

  

Kufuatia hatua hiyo,  Mhe.Sangu amesema  Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ipo katika hatua ya  mwisho wa kuandaa utaratibu huo ambao utakuwa mwarobaini wa namna bora wa kutambua mchango wa vijana hao.

Katika hatua nyingine, Mhe. Sangu amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na hivyo kupelekea  baadhi ya watumishi ambao sio waaminifu kuanza kufuja fedha hizo

Kufuatia hatua hiyo Mhe. Sangu ameielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwabana watumishi hao ili kukomesha tabia hiyo.

Hata hivyo Mhe.Sangu amesema Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kuwasimamia watumishi wote nchini ili kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo zinapopelekwa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo  zinasimamiwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa  

“TAKUKURU hakikisheni mnawabana watumishi ambao  ni wadokozi wa  fedha  za miradi ya maendeleo inayotolewa na Rais wetu” amesisitiza Mhe. Sangu.

Related Posts