Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yaahirisha hukumu ya mapitio ya Kesi ya Mzee Magoma

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Agosti 9, 2024 kutoa uamuzi wa mapitio ya hukumu iliyompa ushindi Mzee Juma Ally Magoma ya kwamba Katiba ya Yanga ya mwaka 2011 ni batili, bali halali ni ile ya mwaka 1968.

Itakumbukwa kuwa mabadiliko ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2011 ilikuwa na miundo tofauti ikiwemo uwepo wa Rais wa Klabu, huku ya mwaka 1968 ikimtaja Mwenyekiti wa Klabu.

Hata hivyo, leo Agosti 7, 2024 Mzee Magoma anayejiita Mwanachama wa Klabu ya Yanga alifika katika mahakama hiyo na wadau wegine wa soka kwa ajili ya kusikiliza mapitio ya hukumu hiyo.

Uamuzi ama hukumu hiyo iliyopangwa kutolewa leo na Hakimu Mfawidhi, Franco Kiswaga unatokana na maombi ya Bodi ya Wadhamini wa Yanga S.C kutaka mahakama hiyo irejee uamuzi wake uliobatilisha Katiba ya Yanga ya mwaka 2011.

Hata hivyo, hukumu hiyo imeshindwa kusomwa leo ambapo imeahirishwa hadi Agosti 9, 2024, huku Mawakili wa Mzee Magoma wakishindwa kufika mahakamani kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Maombi ya marejeo ya uamuzi uliompa ushindi Mzee Magoma yalifunguliwa mahakamani hapo na Bodi ya Wadhamini wa Klabu hiyo wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu uliompa ushindi Mzee Magoma.

Itakumbukwa kuwa Mahakama ya Kisutu ilimpa ushindi Mzee wa Magoma na mlalamikaji namba mbili Geofrey Mwaipopo huku mlalamikaji wa tatu akiwa Jabir Katundu ya kwamba Rais Injinia Hersi Saidi aondoke madarakani kwani uwepo wao haukufuata katiba ya Klabu hiyo.

Inaelezwa kuwa Novemba 6, mwaka 2022, watu wawili walifungua kesi katika mahakama hiyo dhidi ya Baraza la Wadhamini kama mlalamikiwa namba moja, mama Fatma Karume, Abeid Mohamed Abeid, ambaye ni mlalamikiwa namba tatu.

Related Posts