Rais wa mpito wa Bangladesh kuapishwa Alhamis ya Agosti 8 – DW – 07.08.2024

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari yake kwenye uwanja wa ndege wa Paris, na kuelekea Dubai ambapo atapanda ndege nyingine kuelekea Dhaka, Yunus amesema anatarajiwa kurejea nyumbani, kushuhudia kile kinachoendelea na kutafakari wanavyoweza kujipanga kwa lengo la kujikwamua na matatizo walionayo.

Kukiwa na idadi kubwa wa waandishi wa habari na usalama ulioimarishwa Yunus hakuwa na nafasi ya kujibu maswali mengi ya waandishi wa habari waliobahatika kumsogelea. Alipoulizwa lini hasa uchaguzi wa Bangladesh utafanyika jibu lake lilikuwa fupi tu ya kuwa ni mgeni kwa yote yanayoendela kwa hivyo atahitaji muda wa kufanya mazungumzo ili kufikia maamuzi.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli Muhammad Yunus aondoka mjini Paris

Paris | Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Bangladesh na mkuu mpya wa serikali ya mpito Muhammad Yunus
Mshindi wa Tuzo ya Nobel Muhammad Yunus akiwapungia mkono wanahabari katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle huko Roissy, kaskazini mwa Paris, Agosti 7, 2024Picha: Michel Euler/AP/picture alliance

Mshindi huyo wa tuzo ya Nobeli alielekea katika eneo la kuanzia safari yake huku akiiwapa mkono wa kwaheri waliomsindikiza wakiwemo waandishi wa habar akiburuza begi dogo la magurudumu. Huyo ndiye atakaeongoza serikali ya mpito, ikiwa ni baada ya muda mrefu na mtawala wa kimabavu wa taifa hilo Sheikh Hasina kulikimbia taifa hilo.

Ndani nchini Bangladesh, Katibu Mkuu wa cha upinzani chenye nguvu nchini humo cha, Bangladesh Nationalist Party, Islam Alamgir, amesema chama hicho lazima kifanye uchaguzi wake katika kipindi kisichozidi miezi mitatu baada ya Sheikh Hasina kujiuzulu kama waziri mkuu na kuikimbia nchi.

Rais wa mpito wa Bangladesh kuapishwa Alhamis

Wakati upinzani ukihimiza hilo, mkuu wa majeshi wa Bangladesh, Jenerali Waker-Uz-Zaman amesema serikali ya mpito inatarajiwa kuapishwa usiku wa Alhamis, huku Yunus akianza jukumu lake nakurejeshaamani ya nchi baada ya vurugu zilizomuondoa Waziri Mkuu Sheikh Hasina, na kufanya akatafute hifadhi huko India.

Katika hotuba yake kupitia televisheni mchana wa leo Jenerali huyo ametoa ahadi ya wale wote ambao wamehusika na vurugu zilizosababisha Hasina kujiuzulu watafikishwa katika mikono ya sheria.

Mkuu huyo wa kijeshi, akiambatana na wakuu wa jeshi la wanamaji na anga, alitoa uthibitisho wa kuzungumza na Yunus na kueleza kuwa anatarajia kumpokea mteule huyo kwenye uwanja wa ndege wa Dhaka, Alhamis. Jenerali Zaman kadhalika alionesha matumaini ya kwamba Yunus atalipeleka taifa hilo katika mchakato mzuri wa kidemokrasia.

Soma zaidi:Waandamanaji wanasubiri kukamilishwa serikali ya mpito Bangladesh

Zaidi ya majuma matatu ya maandamano ya ghasia ya Bangladesh zimesababisha vifo vya watu wapatao 300 ikiwa ni kabla ya Wazri Mkuu Hasina kuondoka, na takriban wengine 100 waliuawa baada ya vurugu kupamba moto katika maeneo mengi ya nchi baada ya kujiuzulu kwake.

Related Posts