Mkurugenzi huyo ameyasema hayoLeo Jijini Dodoma August 7,2024 katika maonesho ya 88 yanayoendelea Jijini humo ikiwa ni mara baada ya kukagua bidhaa za baadhi ya vukundi vya walengwa wa TASAF ikiwemo Sabuni za kufua na kuoga,Batika na Mikoba.
Na kuongeza kuwa Takwimu za Taasisi ya Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa asilimia 8 ya Watanzania wako katika hali ya umaskini ukiokithili hivyo wao wanawalenga hao.
“Kwa takwimu za NBS inaonesha kwamba asilimia 8 ya Watanzania wako katika umaskini uliokithili,kwahiyo hao ndio ambao sisi tunawalenga”.
Mpaka sasa tunazo kaya takribani milioni 1.3 ambazo tuanendelea kuzisapoti na kati ya hizo tumeshafanya tathmini kwasababu wengi waliingia 2015 wameanza kunufaika na wengine waliingia 2020″.
Pamoja na hayo amesema kuwa wamefanya tathmini kwa walengwa ambao wamekuwa kwa muda mrefu ndani ya TASAF na wameona kuwa hali zao zimeboreka taofauti na awali ambao ni takribani walengwa laki 4.
” Kwahiyo waliokaa muda mrefu tumeshafanya tathmini tumeona hali zao zimeboreka kwakweli ambao takribani walengwa laki 4″.
Pia Mziray ameeleza juhudi wanazofanya ili kuhakikisha wanufaika wa TASAF wanapata soko katika bidhaa zao ambapo amesema wanahakikisha bidhaa zinazotengenezwa zina ubora shindani lakini pia kuwakutanisha wana vikundi taasisi zingine katika mafunzo yao kama vile Sido ili kuona namna gani wanatengeneza bidhaa zenye ubora.
“Ukosefu wa soko ni changamoto ambayo bado tunaifanyia kazi ila tunachoangalia zaidi ili bidhaa za hao walengwa zipate soko zuri,lazima zitengenezwe katika ubora ambao kweli kitu kikienda sokoni kikawa kiko vizuri zaidi”.
“Kwahiyo tunaangalia namna bora ya kuungana na Taasisi nyingine ambazo ziko katika maeneo yao kama vile Sido ili wakati wa kufanya mafunzo kwa vikundi hivi tushirikiane nao kuona namna gani tunatengeneza bidhaa zenye ubora zaidi na zenye ushindani”.
Naye Benno Mgaya kutoka chini ya mwamvuli wa SAIGOT amesema kuwa kwa kushirikiana na TASAF wao wamekuwa wakitoa elimu ya kuwabadilisha mtazamo wakulima kuwa wanaweza kufanya jambo kwa kuanza na hela yeyote iliyopo ili kuondokana na umasimini kwani sio hilo sio neno zuri, ili Serikali itakapokuja kuwashika mkono kwa kuwasapoti wajue nini cha kufanya baada ya kupewa elimu ya kilimo biashara.
“Sisi tunachokifanya ni kunabadilisha wakulima mtazamo kuwa wanaweza kufanya chochote kwa hela iliyopo hata kama ni kidogo ili kuondokana umasikini mana sio neno na limekaa kama tusi, yaani kufanya ushauri nasaha ili Serikali itakapokuja kumshika mkono ajue cha kufanya kwa kupewa elimu ya kilimo biashara “.
“Tangu tuanze hii tunayoita mkulimwa kwa mkulima tumewafikia wakulima 4,780 kwa mikoa 9 yenye kaya maskini ikiwemo Njombe,Ruvuma,Mbeya,Kigoma,Dodoma kidogo na Morogora -Gairo”.
Moja ya kijana aliyetoka katika katika familia ya wanufaika na yeye kuwa mmoja wa wanufaika Habiba Selemani Maramoja kutoka Mbagala Temeka amesema kuwa TASAF imemsaidi sana kwani ilikuwa inatoa ruzuku kwa familia yake na kupelekea kuwa na maisha mazuri na uhakika wa chakula ambapo ni tofauti hapo awali ambapo familia yale ilikuwa haijaingia TASAF chakula kilikuwa ni shida ambako kulipelekea hata kufanya vibaya katika masomo yake.
“Mimi nimeanza kunufaika na mfuko wa TASAF kuanzia 2014 nikiwa kidato cha kwanza mpaka kidoto cha 4 nankufanikiwa kufika chuo kikuu. Mimi mfuko wa TASAF umenisaidia sana kwasababu ulikuwa unatoa ruzuku kwa familia yangu ambayo iliweza kupata mtaji na kufanya biashara kwani kabla maisha yalikuwa magumu kutokana na ukosefu wa pesa ya chakula hivyo nillikuwa naenda shule katika mazingira magumu ambayo yalipelekea kutofanya vizuri katika masomo yangu,sikufanya vizuri darasa la saba kwenda kidato cha kwanza. Lakini baada ya mfuko kutusaidia mzazi alipata mtaji wa biashara ambapo tuliweza kupata chakula pia vifaa muhimu vya shule tofauti na mwanzo,hivyo nikaanza kusoma vizuri na kidato cha 6 nilifanya vizuri sana hivyo TASAF iliniunganisha na Bodi ya mikopo na nilipata mkopo kwa asilimia 100 kwasababu natoka katika familia duni, hivyo Naishukuru sa TASAF kwani bila wao wazazi wangu wasingeweza kwani gharama ya masomo yangi ni kubwa mno”.
TASAF ni mfuko wa maendeleo ya jamii ambao ni program ya Serikali ulioanzishwa kusaidiana na juhudi zjngine za serikali katika kuindoa umasikini.