Deni la Zanzibar ni himilivu -Rais Mwinyi

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakusanya shilingi bilioni 300 kila mwaka kwa kulipa madeni na Serikali inaweza kulipa deni lolote na bado ni himilivu.

Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 8 Agosti 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake alipozungumza na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi , na Majimbo za Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa CCM Mkoa.

Aidha Dkt.Mwinyi amesema Serikali imetekeleza mambo mengi sana ya maendeleo ambayo wananchi waliahidiwa kupitia ilani ya utekelezaji ya CCM mwaka 2020-2025 na itaendelea kutekeleza zaidi.

Halikadhalika Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa atajibu kwa takwimu sahihi hoja zote zinazopotoshwa kwani hakuna jambo la kuficha kwa yanayosemwa yote na Wanasiasa ni uzushi, chuki na uongo.

Vilevile Dkt.Mwinyi amesema ataendelea kudumisha amani nchini kwa maslahi mapana ya Wazanzibari.

Kwa upande mwingine Dkt.Mwinyi amesema ameidhinisha shilingi bilioni 11 za kulipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa bandari ya Mangapwani, alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wachague wao wenyewe kati ya fidia ya fedha au nyumba ambazo zinajengwa na Serikali.

Related Posts