MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu Klabu ya Yanga kufanya mapitio ya marejeo ya shauri la madai namba 187/2022 lililofunguliwa na Juma Magoma na mwenzake Geofrey Mwaipopo.
Pia mahakama hiyo imetupilia mbali mwenendo mzima wa kesi hiyo ya madai namba 187/2022 na kuweka kando amri zote zilizotolewa katika katika hukumu iliyotolewa Agosti 2, 2023.
Pia, mMahakama hiyo imeamuru Magoma, Mwaipopo na Abeid Mohamed Abeid, wailipe Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Yanga, gharama za shauri hilo la mapitio.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa (Agosti 9, 2024) na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga, wakati akitoa uamuzi katika shauri la marejeo namba 17939 yaliyowasilishwa na Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Yanga.
Katika shauri hilo Yanga kupitia wakili wake, Kalaghe Rashid na Respocius Didas waliiomba mahakama hiyo irejee uamuzi uliobatilisha Katiba ya mwaka 2011.
Mahakama hiyo katika uamuzi uliotolewa na Hakimu Pamela Mazengo, Agosti 2, 2023 ilibatilisha Katiba ya sasa ya Yanga ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2011.
Uamuzi huo ulitokana na kesi iliyofunguliwa Agosti 4, 2022 na Magoma na mwenzake Mwaipopo, wanaojitambulisha kama wanachama wa klabu hiyo.
Katika kesi hiyo Magoma na Mwaipopo walipinga Katiba hiyo ya 2011 kuwa si halali kisheria na kwamba Katiba halali inayotambulika ni ile ya mwaka 19868.
Endelea kutembelea mitandao ya kijamii ya Mwanaspoti kwaa taarifa zaidi…