Moshi. Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Shalom Tarimo (21), mkazi wa Msaranga, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima, kilichokuwa kikitumika kuhifadhia mafuta katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kisima hicho katika kituo hicho kinachodaiwa kumilikiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa Moshi, kilikuwa kikifanyiwa ukarabati baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kutumika.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo Agosti 9, 2024 ambapo mwili wa kijana huyo umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mawenzi.
Endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa zaidi.