Msajili wa Hazina akutana na Bosi mpya wa Bodi ya Mikopo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kuzungumza na Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Dk. Bill Kiwia.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Msajili wa Hazina Aprili 25, 2024 jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha kwa Menejimenti hiyo, kufuatia uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa HESLB.

Katika kikao hicho, viongozi hao wawili walijadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuongeza ufanisi na tija kwa kuzingatia falsafa ya R4 ya Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, katika kikao hicho Dk. Kiwia aliwasilisha mikakati yake itakayowezesha taasisi hiyo kufikia malengo yake ya kuhakikisha vijana wengi wa kitanzania wanatimiza ndoto zao za kusoma elimu ya juu kwa kunufaika na mikopo wanayoitoa kwa manufaa ya jamii zao na Taifa kwa ujumla.

Related Posts