CRDB BENKI IMEKOPESHA SHILINGI TRILIONI 4. 06 SEKTA YA KILIMO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima almaarufu kama Nanenane yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma, kwa miaka mitatu iliyopita hadi Julai 2024, Benki ya CRDB imesema imekopesha jumla ya shilingi trilioni 4.06 kwenye sekta ya kilimo huku zaidi ya shilingi trilioni 1.81 ambazo ni sawa na asilimia 43 ya mikopo yote iliyotolewa na taasisi za fedha kwenye sekta ya kilimo nchini, zikitolewa katika msimu huu wa kilimo.

 

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amemweleza Mheshimiwa Dkt. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa shilingi bilioni 944.6 kati ya kiasi hicho, zimeelekezwa kwenye vyama 541 vya ushirika (AMCOS) kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo, ujenzi wa maghala na viwanda vya kuchakata mazao, ufugaji, uwekezaji kwenye misitu, na uvuvi.

 

 

 

Kwenye sekta ya mifugo na uvuvi, mpaka Julai 2024, amesema Benki ya CRDB imekopesha shilingi bilioni 70 na tumeingia makubaliano na Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutoa mikopo kwa wanachama wake ili wafuge kwa tija kwa kuweka miundombinu ya kunyweshea na kulima chakula cha mifugo.

 

 

 

Kule Zanzibar, Benki ya CRDB inatekeleza mpango maalum wa Inuka na Uchumi wa Buluu ambao hadi Julai 2024, imeshakopesha zaidi ya shilingi bilioni 29 kwenye Programu ya Inuka kwa wajasiriamali na shilingi bilioni 28 kwenye uchumi wa buluu.

 

 

 

 

Nsekela pia ameielezea Programu ya Imbeju inayotekelezwa na taasisi yake ya CRDB Bank Foundation ikijikita kuwawezesha vijana, wanawake na makundi maalumu wakiwemo wakulima na wafugaji kwa kuwapa elimu ya fedha, mafunzo ya ujasiriamali

Related Posts