WASHIRIKI INEC WALA KIAPO CHA UTII – MWANAHARAKATI MZALENDO

Washiriki wa Mafunzo yaliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Shinyinga wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Mafunzo hayo yameanza leo tarehe 10 Agosti, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga. Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Shinyanga utafanyika sambamba na Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 21 hadi 27, Agosti, 2024 ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni (PICHA NA INEC).

#KonceptTvUpdates

Related Posts