Rais Samia kuhudhuria kuapishwa kwa Kagame kesho

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Rwanda, Paul Kagame.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Agosti 10, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasilinao ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga, imesema Rais Samia atasafiri kesho asubuhi kuelekea Rwanda kwa ajili ya shughuli hiyo itakayofanyika Agosti 11, 2024.

Kagame alichaguliwa tena kuwa Rais wa nchi hiyo Julai mwaka huu kwa ushindi wa asilimia 99.15 ya kura.

Wagombea wengine katika uchaguzi huo walikuwa Frank Habineza  wa Democratic Green Party aliyepata asilimia 0.53 na Philippe Mpayimana aliambulia asilimia 0.32.

Baada ya kuapishwa Kagame atakuwa na miaka mingine mitano kama kiongozi wa nchi hiyo tangu yalipokoma mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nabaadaye akawa Rais tangu 2000.

Related Posts