KTO YAWAFIKIA VIJANA TAKRIBANI ELFU 17 NCHINI KATIKA MIRADI YAKE MITATU IKIWEMO YA MPIRA FURSA.

Na MWANDISHI wetu Dodoma

MKURUGENZI wa Karibu Tanzania Organisation (KTO), Maggid Mjengwa amesema kuwa wameweza kuwafikia vijana wapatao Elfu 17 hapa Nchini katika zao za Elimu haina mwisho,Mpira fursa na SD ambayo inasimama katika malezi na makuzi ya watoto.

Maggid ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma wakati akizungumza na Wanahabari mara baada ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya siku ya vijana Kimataifa yanayofanyika Jijini hapa ambapo KTO ni moja katika ya Taasisi mbalimbali zinazoonesha bunifu mbalimbali katika viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete.

“Tuna vijana wapatao 17 elfu kwenye vyuo vya Maendeleo ya wananchi na katika hao kuna wanaopitia kwenye program ya Elimu haina mwisho,Mpira fursa na SD kwa maana ya kufanya kazi kwenye vituo vya kulelea watoto,lakini pia kuna watu takribani elfu 4 ambao wamehitimu kupitia Program zetu”.

Aidha amezungumzia moja ya mikakati ya KTO katika kuhakikisha inapambana na changamoto ya ajira kwa vijana ambapo amesema jambo ambalo KTO inafanya ni pamoja na kuwepo kwa program ya mpira fursa ambayo imeweza kutoa vijana ikiwemo moja ya Refa ambaye yupo katika viwango vya TFF.

“Moja ya jambo ambalo tunalifanya kupitia program ni kutatua hiyo changamoto ya ajira ni kupitia Program ya mpira fursa ,utaona tunaye mmoja hapa ambaye ni refa baada ya kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi,hivyo utaona sio kucheza tu mpira tu mpira lakini hata kuwa refa au kuwa kocha yote hiyo inatokana na program hii ya Mpira fursa”.

Pia Mkurugenzi huyo amesema kuwa KTO ni Taasisi isiyo ya serikali lakini inafanya kazi na serikali na kuweza kutoa program zao hizo 3 ikiwemo elimu haina mwisho inayolenga vijana wanawake waliokatishwa masomo kwa sababu mbalimbali kama ujauzito,ndoa za utotoni na umasikini.

“Sisi KTO tunafanyakazi na vyuo na katika vyuo hivyo sisi kama taasisi isiyo ya kiserkali inayofanyakazi na serikali tuna program 3 ikiwemo elimu haina mwisho ambayo inalenga vijana wanawake waliokatishwa masomo kwasababu mbalimbali ikiwemo ujauzito,ndoa za utotoni na umasimini,pili program inayohusina na masuala ya malezi,makuzi na maendeleo ya watoto na program ya 3 tunayofanya na vyuo hivyo ni mpira fursa hapa wanajifunza kutengeneza mipira ya yenye viwango vya hali ya juu,ukocha,Urefa na tiba za kimichezo katika vyuo vyote 54 vya maendeleo ya Wananchi”.

Naye moja ya Kocha wa Mpira fursa Bi Johnither Kabunga amesema kuwa program hii imesaidia kwa asilimia kubwa kijana kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwani wameweza kupata mabinti wanaocheza mpira wa miguu na kupata waamuzi ambao wameweza kufika kiwango cha Data Base za TFF.

“Kupitia program ya mpira fursa ambayo ni kukuza nankuendeleza soka la wanawake imesaidia kwa asilimka kubwa kijana kutoka sehemu moja kwenda nyingine,tuna mabinti ambao wanacheza mpira wa miguu kupitia program hii,tumepata waamuzi ambao wamefikia kiwango cha kufikisha kwenye data base za TFF, hivyo vijana wengi wameongeza hamasa ya kucheza mpira,hivyo niseme mpira ni zaidi ya kawaida,mpira ni fursa,mpira ni ajira,mpira ni burudani”.

Moja ya mnufaika wa program ya Mpira Fursa Tulizo Mwatwebe ambaye ni mwamuzi pia ametumia wasaa huu kutoa wito kwa mabinti walioko majumbani kwa wale waliokatisha masomo kwamba bado wana fursa kubwa kwani Taasisi inatoa elimu kwa wote hivyo bado hawajapoteza kikubwa ni kujipanga na kurudi shule kama ilivyokuwa kwake baada ya kukatisha masomo alikuwa na ndoto ya kuendelea akakutana KTO akaendelea na masomo kupitia progra ya elimu haina .wisho na kuweza kupata fursa mbalimbali ikiwemo kupata mafunzo katika chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.

“Wito wangu ni kwa wale mabinti ambao wako nyumbani kwamba bado wana fursa kubwa,kwasababu hili Shirika linatoa elimu kwa watu wote hivyo bado wana nafasi hawajapoteza chochote lengo ni kujipanga na kurudi shuleni wapate mafunzo yao lakini wana uwezo pia wa kuendelea mbele zaidi”.

“Baada ya kukatisha masomo lakini bado nilikuwa na ndoto na nilitamani nirudie masomo yangu ili nimalize kidato cha 4 na kuendelea,ndipo nikapata fursa hiyo hapa KTO katika program ya elimu haina mwisho kwahiyi nikanufaika na hiyo program na nikafanya mtihani wa kidato cha 4 na nilipomaliza nikaomba kjiunga na chuo cha maendeleo ya michezo Malya nikapata na sasa nipo nasoma huko”.

KTO inafanyakazi na vyuo 54 nchini vilivyochini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.



Related Posts