ONGEA NA AUNT BETTIE: Umeamua kuwa hawara wa kudumu komaa

Anti ninashindwa hata nianzie wapi kwa haya ninayopitia kwa mwanamume ninayeishi naye.

Kabla sijaeleza changamoto yangu, naomba ujue ninampenda, ninaipenda familia yake na siwezi kutoka licha ya maswahiba ninayopitia.

Tunaishi wote huu mwaka wa 12, hajawahi kuzungumzia kunioa, licha ya kumlelea watoto wake wawili waliotelekezwa na mama zao, mmoja ana miaka mitatu na mwingine mitano. Hawa hivi sasa ni wakubwa na wanaendelea na masomo.

Pia kuna wadogo zake watatu niliwakuta wanasoma, hivi sasa wawili wanafanya kazi na mmoja bado nipo naye hapa nyumbani.

Lakini ameamua kunifanya hawara wa kudumu, hajawahi kuzungumzia kunioa hata kwa ndoa ya kimila kwa maana ya kwenda kujitambulisha kwetu na kutoa mahari. Nashindwa nifanyeje, nimechoshwa na hali hiyo, kwani inanifanya hata nyumbani hawanielewi.

Nami pia ninashindwa hata nianzie wapi, nianze kwa kukusema wewe mwenyewe kwa kukubali kuwa hawara wa kudumu, niwaseme kwenu kwa kukubali mtoto wao achezewe kwa miaka 12 au nimseme mpenzi wako kwa kuamua kuwa mpenzi wa kudumu.

Naanza na wewe mwenyewe, kwani ndiyo mwamuzi wa hili jambo, si wazazi wako unaosema hawakuelewi wala hawara yako wa kudumu. Umeishi na mtu zaidi ya miaka 10 hajazungumzia kukuoa na wewe umekaa kimya, ina maana umekubaliana na hilo jambo.

Kweli kuolewa si lazima kidunia, lakini kiimani ni lazima na kiheshima pia ni muhimu, kama unavyosema hata kwenu hawakuelewi.

Inawezekana anaishi na wewe kwa sababu unamlelea watoto na ndugu zake, lakini ana mipango ya kumuoa mwanamke mwingine afanye naye maisha na ndiyo maana amekaa kimya. Au anajua hutaki kuolewa kwa sababu umekaa kimya miaka inakatika. Vunja ukimya, mueleze mnavyoishi si sawa, mnapaswa kuoana. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamume ndiye anapaswa kumwambia mwanamke kuhusu masuala ya ndoa, kama amekaa kimya mwambie wewe kwa sababu ndoa ni ya watu wawili, si ya mmoja kwamba peke yake ndiyo anapaswa kuamua.

Ukimueleza ndiyo utajua kama anakupenda kweli au ameamua kukufanya hawara wa kudumu. Angalia usije kuwa unaishi na mwanamume wa watu katika nyumba yake.

Yaani unaishi naye analala na kuamka akiwa na wewe, kumbe ana mke na watoto mahali kwingine, wewe umebaki kulea ndugu na watoto. Nakupongeza kwa malezi, lakini usijinyime haki yako ya kuwa mke.

Zungumza naye upate jibu la maswali yako akikusikiliza na kutekeleza ujue mpo pamoja, akiwa mbogo, hataki mjadili hilo suala fikiria vinginevyo. Kama umeamua kuwa hawara wa kudumu kwa kukaa kimya, komaa na hayo maisha.
Sitaki huruma zake zisizo na msingi tukiwa faragha.

Nina mpenzi ambaye anatarajia kufunga naye ndoa mapema mwakani. Ila ninahisi kuna jambo halijakaa sawa ninapojamiiana naye.
Ana shida moja ya kunihurumia tunapokutana kimwili, yaani anafanya kila awezalo kujamiiana nami kama mtoto mdogo, jambo linalonikera sana. Nitakupa sababu kwa nini linanikera ili uelewe.

Kwanza hakunikuta msichana, nilikutana naye nikiwa tayari nimeshaanza hayo mambo, kwa hiyo kuna vitu ninavijua, ninavipenda na ninajua vinafanyika.
Pili, siyo kama ninamsemea huyu mchumba wangu, bali ninajua kibinadamu kuna mahali huwa anakwenda kupiga shoo shoo, mimi ananifanyia unafiki nisioutaka.

Tatu, ninapenda nikishughulikiwa iwe shughuli ya kisawasawa na si mzaha kama anavyonifanyia.

Changamoto yangu ni namna ya kutoka hapa tulipo ukizingatia ananichukulia wa mkoani, kwani nilikuja mjini chuo nikakutana naye nikiwa bado ninanukia mkoani. Anachosahau hayo mambo hayana wa mjini wala kijijini, inategemea tu ulikutana na watu wa aina gani ulipokuwa unaianza hii safari ndefu yenye visa na mikasa.

Kibaya zaidi hata nikijitahidi kumuonyesha kwa vitendo havifuatilii, nimemsoma anaamini mimi ni mshamba akinipeleka puta nitamchukia kwa kuwa ananipenda sana.

Huu uaminifu wake kwangu, kunihurumia bila sababu, kunichukulia poa kunanikera sana, kwa sababu kuna siku nakosa hata usingizi.
Unaweza kwenda kwake Ijumaa, mpaka unaondoka Jumapili hajakukata kiu, kazi yake kunibembeleza, kuninunulia zawadi na kunitoa ‘out’, kunining’inia nitakavyo aah.

Halafu ana kila sifa za kufanya hivyo, pumzi anazo na mwili wa matumizi hayo anao pia. Ananifanya niwe na wivu, kwani naamini kuna mahali huwa anakwenda kucheza mechi, kwangu anapiga jalamba.

Nisaidie nifanyeje aelewe kuwa sihitaji huruma zisizokuwa na sababu?
Kwanza nicheke. Nakuunga mkono kabisa, hakuna haja ya kuhurumiana, mkiamua kulianzisha lianzisheni kwa kadiri ya mapenzi na uwezo wenu.
Ila hili wa kwetu umelilea mwenyewe, inawezekana siku za mwanzo mlivyokutana ulikuwa unajiliza liza na kwa kuwa anakupenda hataki kukupoteza.

Wasiwasi wako kuhusu kwenda nje kupiga shoo kali sina shaka nao, inawezekana kabisa, hataki vilio vyako visivyojulikana vya mahaba au maumivu na uchovu.

Kuanzia sasa vibe litoke kwako, kwanza usisubiri akuanze, ikiwezekana mkikutana anzia mlangoni kumuonyesha unachohitaji. Muonyeshe majonjo ajue kama segere unaliweza, achana na mambo ya kujifunika funika kulialia vilio visivyoeleweka.

Jihudumie, jipimie, akiacha usimuache, ukiwa na hamasa naamini hatakuwa na nafasi ya kusubiri kwenda kupiga shoo kwingine.

Akijifanya kukuhurumia kasirika, endelea kupambana akupe huduma unayostahili. Inawezekana unawaza anaweza na anakwenda kwingine kumalizia haja zake, kumbe hapo kwako ndiyo amemaliza.

Usimwambie kwa maneno, inawezekana unaona aibu ukizingatia umekulia huko zilikozaliwa hizo aibu, mwambie kwa vitendo.

Akilala muamshe, akichoka toka naye nje akapate hewa safi kidogo, akiende bafuni mfuate ilimradi ajue hautanii. Sasa usimfuate kama vita, mfuate kimahaba, naamini anakuelewa mapema sana.

Yale machejo unayosema hata kijijini yapo yatumie sasa. Muhimu zaidi kuwa sehemu ya huu mchezo, tawala jukwaa, hivyo hakikisha unajua ukimgusa wapi anakuwa anatamani kuingia uwanjani.

Tofauti na hapo utakuwa unalalamika tu, usipompa vibe atakuwa anakugusagusa, mwenzio anajua wa kijijini hawataki mieleka, kumbe amekutana na mwanamasumbwi kabisa anayetaka pambano la kimataifa.
 

Kila akinitafuta ananipiga mzinga, nimechoka

Ninafanya kazi nje ya mkoa ilipo familia yangu kwa maana ya mke na watoto wangu.
Tatizo lililonifanya nikutafute Anti uniulizie na kwa wenzangu hivi mwanamke anapaswa kumtafuta mumewe wakati gani?

Maana huyu wangu kama hana shida hanitafuti kabisa, niliweka utaratibu mshahara wangu unapotoka pesa inayoingia kwake inakatwa moja kwa moja na kuingizwa kwenye akaunti yake anaweza kuzipata hizo pesa ana asiseme. Ila zikipungua ndiyo atanitafuta kutwa nzima.

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa hajawahi kunitafuta bila kuwa na shida, kama siyo ya kutaka pesa basi ananiaga anataka kwenda mahali.

Lazima awe na jambo na si kunisalimia tu kama mimi ninavyofanya, ndiyo maana naomba uniulizie kwa wadau wako au unieleweshe hii ni sawa?

Kiuhalisia si sawa, mkeo anakuchukulia poa, labda kwa sababu upo mbali. Ila ninavyojua wapendanao hupigiana simu bila sababu za msingi ilimradi kila mmoja amemkumbuka mwenzake, tena nyinyi mnaoishi mbalimbali ndiyo kabia kukumbukana ni karibu kila siku.

Ila sijui hapo awali wakati mnaishi pamoja ilikuwaje, pengine mlikuwa hamtafutani mchana kila mmoja anafanya shughuli zake mtakutana jioni au hamkuwa watu wa stori, hivyo hajui akikupigia akuambie nini ndiyo maana hufanya hivyo akiwa na jambo.

Ila hujachelewa muulize kwa nini anafanya hivyo, pengine ana sababu. Akikujibu ana sababu utajua wapi pana shida, akikujibu hana sababu ni jukumu lako kumfundisha siku nyingine awe anakupigia simu kukusalimia. Mweleze umeimiss salamu yake isiyoambatana na mahitaji. Hapo utakuwa umeuondoa huu utata.

Related Posts