Vijana elfu 45 kujikomboa kiuchumi KUPITIA ujasiriamali

Imeelezwa kuwa ukosefu wa ajira Kwa vijana ni chanzo Cha vijana wengi nchini kujiingiza katika vitendo vya kihalifu ikiwemo Wizi,utumiaji dawa za kulevya na magenge yasiyofaa na kupelekea wengine kuishia katika vifungo jela.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo ya ajira zaidi ya vijana elfu 40 kutoka Dar es Salaam,Morogoro na Zanzibar wanatarajia kunufaika na kujikomboa kiuchumi kupitia Taasisi ya Tanzania Youth Coalition (TYC) chini ya mradi wa USAID Kijana Nahodha (Young Captain) unaofadhiliwa na USAID na mradi wa Boresha Maisha ya Vijana unaofadhiliwa na WE EFFECT.

Akizungunza na Ayo tv na Millard ayo .com afisa miradi taasisi hiyo Domitila Jonace,amesema lengo la mradi wa Boresha Maisha ya Vijana unaotekelezwa katika mikoa ya Iringa,Mwanza,Dodoma na Kilimanjaro ni kuwapatia ujuzi vijana kwenye masuala ya ujasiriamali, elimu ya afya na utawala Bora.

Amesema,endapo vijana watapatiwa elimu ya ujasiriamali wataweza kujikomboa kiuchumi Kwa kufanya shughuli mbalimbali sambamba na kutumia vizuri mikopo ya asilimia 10 ya vijana ,wanawake na walemavu ambayo inatolewa na halmashauri.

Naye Salma Kagya afisa programu wa taasisi ya TYC amesema, mradi wa USAID Kijana Nahodha(Young Captain) unawafikia vijana katika mikoa ya Morogoro,Dar es Salaam na Zanzibar ukiwa na lengo kuu la kumuongezea uwezo kijana katika uzalishaji mali,kujitambua,afya na ushiriki na ushirikishwaji bora katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Aidha suala la afya na demokrasia ni miongoni mwa mambo yanayotolewa kipaumbele kwenye miradi hiyo ili vijana waweze kujali afya zao kuwa na nguvu Kazi

Nao baadhi ya wanufaika wamelishukuru shirika hilo kwa kuwawawezesha ambapo wanaamini watajikomboa kiuchumi na kuacha masuala ya kuwa tegemezi.

 

 

 

Related Posts